Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkuu wa haki za binadamu wa UM ameanza ziara Senegal na Guinea:

Mkuu wa haki za binadamu wa UM ameanza ziara Senegal na Guinea:

Kamishina mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Navi Pillay yuko katika ziara yake ya kwanza Afrika ya Magharibi . Kuanzia tarehe 13 Machi nahdi kesho Jumanne March 15 atakuwa nchini Guinea kabla ya kuelekea senegal atakakokuwa hadi Machi 18.

Katika ziara hii atakuna pia na viongozi wa serikali wa nchi zote mbili na jumuiya za kijamii kujadili masuala ya haki za binadamu. Nchini Senegal ambako kuna makao makuu ya ofisi ya haki za binadamu kwa nchi za Afrika ya Magharibi Bi Pillay atakutana na Rais Aboulaye Wade, mawaziri, mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Afrika Magharibi, jumuiya za kijamii na wanaharakati wa haki za binadamu.