Skip to main content

Burundi bado ina kibarua kigumu katika kuleta usawa wa elimu na masuala ya mirathi

Burundi bado ina kibarua kigumu katika kuleta usawa wa elimu na masuala ya mirathi

Wiki hii ulimwengu umeadhimisha siku ya kimataifa ya wanawake hapo machi 8, na Burundi imeungana na jumuiya ya kimtaifa kusheherekea siku hiyo ambapo pia mwaka huu ni miaka 100 tangu kuanza kuadhimishwa siku hiyo kimataifa.

Pamoja Burundi kupiga hatua kubwa katika uwakilishi wa wanawake kwenye taasisi za uongozi wa taifa kwa kuwa na asilimia 30 ya wanawake katika serikali, bado kuna kazi kubwa ya kuwakomboa wanawake hasa kinamama wa vijijini .

Kauli mbiu ya mwaka huu imekuwa ni fursa ya elimu,sayansi na teknolojia ambalo ni daraja la kuwavusha wanawake kupata ajira bora. Hata hivo kwa nchi ya Burundi taakwimu zaonyesha kuwa itakuwa ni ndoto kufikia lengo hilo la milenia mnamo miaka minne ijayo kabla ya 2015.

Mbali ya usawa katika elimu wanakabiliwa na changamoto nyingine, ambayo ni sheria kuhusu mirathi ambapo mwanamke wa vijijini hana haki ya urithi kama alivyo mwanaume. Ili kuchambua mengi kuhusu hayo, mwandishi wetu wa Bujumbura Ramadhani KIBUGA ametuandalia makala hii, Ungana naye.

(MAKALA NA RAMADHAN KIBUGA)