Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nataraji kupunguza machungu kwa Walibya:Al-Khatib

Nataraji kupunguza machungu kwa Walibya:Al-Khatib

Mwakilishi mpya aliyeteuliwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Libya anatumai kumaliza mateso na machungu kwa watu wa Libya.

Mwakilishi huyo waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Jordan Abdel Ilah Al-Khatib amezungumza na waandishi wa habari mjini New York hii leo wakati machafuko ya kuuondoa utawala wa Qadhafi yakiendelea .

Al-Khatib amesema kazi yake ni ngumu lakini antaraji kwa niaba ya Umoja wa Mataifa atafanikiwa kusitisha mauaji na kumaliza mateso yanayowakabilia raia wa Libya, na pia kushughulikia mahitaji yao ya haki za binadamu.

Amesema kutimiza lengo hilo ni muhimu ili kuwasaidia Walibya kuchagua hatma yao. Al-Khatib akiwa Libya atakutana na pande zote zinazohusika kwenye machafuko ili kuelewa hali halisi.