Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Libya huenda ikakumbwa na upungufu wa chakula:WFP

Libya huenda ikakumbwa na upungufu wa chakula:WFP

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP limesema Libya huenda ikakabiliwa na upungufu mkubwa wa chakula katika miezi minne ijayo.

Libya ni muagizaji mkubwa wa chakula kutoka nje na machafuko yanayoendelea yamevuruga mipango ya uingizaji chakula. Tathimini ya WFP ndani ya nchi hiyo inaonyesha kwamba akiba ya chakula hivi sasa huenda ikatumika yote katika miezi minne ijayo.

Kwa mujibu wa msemaji wa WFP Emilia Casella tani 1200 za ngano zimewasili Mashariki mwa Libya kulisha watu takriban 90,000 kwa mwezi mmoja na msaada zaidi utawasili wiki ijayo.

(SAUTI YA EMILIA CASELLA)