Bajeti ya UM itapungua kwa asilimia 3 mwaka 2012-2013:Ban
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema bajeti ijayo ya Umoja wa Mataifa itapungua kwa asilimia tatu kwenye kutoka kwa bajeti ya sasa ya miaka miwili ambayo ni dola bilioni 5.16 kutokana na matatizo ya uchumi yanayoikumba dunia.
Amesema uchumi wa dunia safari hii umejikuta katika hali mbaya tangu kuporomoka pakubwa kwa uchumi duniani kulikotokea miaka ya 1930. Akizungumza na maafisa wa bajeti mjini ya mwaka 2012-2013 mjini New york Ban amesema Umoja wa Mataifa lazima uzingatie hali ya sasa ya uchumi katika shughuli zake. George Njogopa na ripoti kamili.