Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uchina na Urusi kuongoza juhudu za UM kupambana na uharamia

Uchina na Urusi kuongoza juhudu za UM kupambana na uharamia

Uchina na Urusi wanaongoza juhudi mpya kwenye Umoja wa Mataifa kukabiliana na tishio la uharamia kwenye pwani ya Somalia na kuushinda mtandao unaohusiana na magaidi wa Al-Qaeida unaodhibiti taifa hilo la pembe ya Afrika.

Urusi imesambaza mswada wa azimio ambao unalitaka baraza la usalama kuanza mara moja mazungumzo ya kuanzishwa kwa mahakama tatu kushughulikia kesi za uharamia. Hatua zingine zitakuwa ni kujengwa kwa magereza mawili kwa ajili ya maharamia watakaokutwa na hatia na wanataka mataifa yote kupitisha sheria za kuufanya uharamia kuwa kosa la jinai.

Balozi wa Urusi kwenye Umoja wa Mataifa Vitaly Churkin amesema lazima suala hili lifikiriwe kwa kina na kupewa uzito mkubwa. Leo hapa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa baraza la usalama linajadili suala la Somalia, na hasa mikakati ya kuhakikisha amani na usalama vinapatikana.