Tanzania kufaidika na mkopo wa kuinua uchumi vijijini:

Tanzania kufaidika na mkopo wa kuinua uchumi vijijini:

Mfuko wa Umoja wa Mataifa wenye lengo la kupambana na umasikini vijijini IFAD leo umesema umetoa mkopo wa dola milioni 90 kwa serikali ya Tanzania ili kuimarisha huduma za kifedha, masoko na kuchagiza maendeleo ya sekta binafsi katika taifa hilo la Afrika ya Mashariki.

Mkopo huo ambao utasaidia miundombinu ya masoko na mipango ya misaada ya fedha vijijini kwa mujibu wa IFAD unatolewa kwa nchi kwa masharti maalumu.

Kilimo kinatambulika kuwa ni uti wa mgongo wa ukuaji wa uchumi wa Tanzania , klakini thamani yake bado haijadodoswa kwa kina na kuleta mafanikio makubwa ya kupunguza umasini vijijini

IFAD inasema wakulima wadogowadogo bado hawawezi kupata mikopo, masoko na fursa ili kuchangia pakubwa maendeleo, hivyo mkopo huo unatumainiwa kusaidia katika Nyanja hiyo.