Skip to main content

Ingawa kuna mafanikio kiasi bado zinahitajika juhudi kumkomboa mwanamke

Ingawa kuna mafanikio kiasi bado zinahitajika juhudi kumkomboa mwanamke

Ingawa sasa ni miaka 100 tangu kuaanza kuadhimishwa rasmi siku ya kimataifa ya wanawake duniani bado kuna juhudi zinazohitajika kuhakikisha mwanamke amejikombia kiuchumi, kisiasa na kijamii.

Wito umekuwa ukitolewa kutoka kila pembe ikiwemo Umoja wa Mataifa katika kuzitaka serikali duniani kubadili sera, na mipango yake ya maendeleo kwa kujumuisha nafasi ya mwanamke na kutambua mchango wake.

Kauli mbiu ya mwaka huu ni fursa katika elimu, sayansi na teknolojia kama silaha ya kumfanya mwanamke kuwa na ajira bora. Kila nchi kuna mafanikio na mapungufu, je nchini Tanzania mambo yakoje? Haya ni maoni ya baadhi ya raia.

(SAUTI ZA WATANZANIA)