Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkutano kupambana na umasikini kufanyika Brazili

Mkutano kupambana na umasikini kufanyika Brazili

Afisa anayehusika na masuala ya uchumi na ya kijamii kwenye Umoja wa Mataifa amesema kuwa mkutano kuhusu maendeleo ambao utaandaliwa mjini Rio de Janeiro nchini Brazil mwaka ujao utatoa fursa nzuri ya kuwasaidia watu kutoka kwenye umaskini.

Sha Zukang aliye pia katibu mkuu kwenye mkutano huo amesema kuwa wanachama wa Umoja wa Mataifa wametambua malengo matatu makuu ya mkutano huo yakiwemo kuwepo kwa maendeleo ya kudumu, kutambua mianya iliyopo na changamoto mpya.

Mkutano wa Rio wa mwaka 2012 unafanyika miaka ishirini baada ya mutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu mazingira na maendeleo kundaliwa mji huo huo wa Rio de Janeiro ambapo mataifa yaliafikiana juu ya kutilia maanani suala ya maendeleo ya kiuchumi na maisha mema ya baadaye kwa wote.