Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Waziri wa zamani wa Kenya anasema yuko tayari kwenda ICC

Waziri wa zamani wa Kenya anasema yuko tayari kwenda ICC

Mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC imewataka watuhumiwa sita wanaoshukiwa kuhusika kwenye ghasia za baada ya uchaguzi mkuu uliokumbwa na utata mwaka 2007 nchini Kenya kufika mbele yake.

Washukiwa hao wakiwemo mawaziri wawili waliochishwa kazi, naibu waziri mkuu na aliyekuwa mkuu wa polisi wanatakiwa kufika mbele ya mahakama ya ICC mnamo tarehe saba mwezi Aprili mwaka huu kujibu mashataka ya kuhusika kwenye ghasia hizo.

Mmoja wa washukiwa hao waziri wa zamani wa viwanda Henry Kosgei anasema kuwa yuko tayari kufika mbele ya mahaka ya ICC kujibu mashtaka yanayomkabili.

(SAUTI YA HENRY KOSGEY)

Takriban watu 1200 waliuawa kwenye ghasia hizo na zaidi ya wengine 500,000 kulazimika kuhama makwao . Baadhi ya washukiwa hawa ni wafuasi wa rais mwai kibaki pamoja na Raila Odinga ambaye kwa sasa ni waziri mkuu kwenye serikali ya muungano.