Skip to main content

Kamati ya maandalizi ya Rio 2012 yakamilisha kikao

Kamati ya maandalizi ya Rio 2012 yakamilisha kikao

Mkurugenzi mtendaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la mazingira UNEP Achim Steiner amesema maendeleo endelevu na mfumo wa ufuatiliaji wa suala hili visichukuliwe kama nguzo tatu zinazofanya kazi peke yake bali kama mfumo wa msokoto.

Ameyasema hayo wakati wa kuhitimisha mkutano wa siku mbili wa kamati ya maandalizi iliyokuwa ikijadili mada mbili kuu za mkutano wa Rio de Janeiro mwaka 2012.

Mada hizo zinajikita katika mabadiliko ya mfumo wa utendaji katika maendeleo endelevu na kuanzisha uchumi unaojali mazingira kwa maendeleo na kutokomeza umasikini mambo ambayo yatakuwa kiini cha malengo ya mkutano utakaofanyika June 2012 nchini Brazili.