Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Pande zinazopigana Afghanistan lazima zihakikishe zinawalinda raia:Ripoti ya UM

Pande zinazopigana Afghanistan lazima zihakikishe zinawalinda raia:Ripoti ya UM

Pande zinazopigana nchini Afghanistan lazima ziongeze juhudi za kuwalinda raia mwaka huu 2011 umesema mpango wa Umoja wa Mataifa nchini humo UNAMA na tume huru ya haki za binadamu nchini Afghanistan katika ripoti yao ya mwaka 2010 ya ulinzi wa raia katika maeneo ya vita.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo wanamgambo waliua raia wengi Afghanistan mwaka jana kuliko wakati mwingine wowote kwa kutumia mabomu yaliyotegwa barabarani, mashambulio ya kujitoa muhanga na mauaji ya kundi kubwa la watu ilipowezekana.

Mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya haki za binadamu katika migogoro Ivan Somonovic amesema kutokana na kuongezeka kwa machafuko na matumizi ya mambomu na mashambulizi ya kujitoa muhanga raia wa Afghanista wamelipa gharama kubwa ya maisha yao mwaka 2010 hivyo kuwalinda ni muhimu sana.

(SAUTI YA IVAN SOMONOVIC)