Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watu 500,000 wathirika na machafuko Ivory Coast

Watu 500,000 wathirika na machafuko Ivory Coast

Karibu watu nusu milioni wamesambaratishwa na machafuko ya kisiasa yanayoendelea nchini Ivory Coast yamesema mashirika ya misaada ya Umoja wa Mataifa.

Katika mji mkuu Abijan watu laki tatu wamelazimika kuzikimbia nyumba zao na Magharibi mwa nchi idadi ya wakimbizi wa ndani imeongezeka na kufikia 70,000.

Shirika la wakimbizi UNHCR na lile la uhamiaji IOM yamesema hali ya kibinadmu inazidi kuwa mbaya na wameyataka makundi kuepuka kuyaweka maisha ya raia hatarini. Adrian Edward ni kutoka UNHCR.

(SAUTI YA ADRIAN EDWARD)

IOM imesema vitendo vya kuwalenga wafanyakazi wa misaada imefanya kuwa vigumu kufikisha msaada kwa wanaouhitaji na kutokana na machafuko limeondoa wafanyakazi wake wa kimataifa kutoka Magharibi mwa Ivory Coast.