Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maelfu ya Watunisia wakimbilia Lampedusa Italia:IOM

Maelfu ya Watunisia wakimbilia Lampedusa Italia:IOM

Boti zingine tisa zilizobeba wahamiaji 660 wote kutoka Tunisia zimewasili kwenye kisiwa cha Lampedusa nchini Italia jana usiku.

Kwa mujibu wa shirika la kimataifa la uhamiaji IOM watu hao wamekimbia nchini Tunisia na kuwasili kwao kumefanya idadi wa wahamiaji kwenye kisiwa cha Lampedusa waliowasili tangu Jumapili kuwa zaidi ya 1500 na wengine wapatao 8000 waliwasili wiki tano zilizopita.

Sasa hali ya bahari imechafuka na wahamiaji wameanza kupungua. Alice Kariuki na ripoti kamili.

(RIPOTI YA ALICE KARIUKI)

Ingawa idadi ya wahamiaji ilikuwa kubwa lakini kuchafuka kwa bahari kumesababisha kupungua kwa wahamiaji kutoka Tunisia wanaowasili kisiwa cha Lampedusa ambacho hapo nyuma kimekuwa kikishuhudia kuwasili kwa hadi wakimbizi 5000 kwa muda wa siku tatu tu. Wakimbizi wote waliowasili walipelekwa kwenye kituo cha kuwapokea wakimbizi walikopewa usaidizi.

Wahudumu kutoka mashirika ya IOM , UNHCR pamoja na UNICEF wanaendelera kuwahudumia wakimbizi hao kwa njia ya ushauri. Hata baada ya jitihada za serikali ya Italia za kuwahamisha wahamiaji hao kwenda kwa vituo vingine bado kituo cha Lambedusa kinaendelea kukabiliwa na idadi kubwa ya wahamiaji.