Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wahamiaji wa Afrika wanasumbuliwa Libya:UNHCR

Wahamiaji wa Afrika wanasumbuliwa Libya:UNHCR

Mashirika la misaada ya kimataifa yameendelea kutiwa hofu na vitendo vya ghasia na ubaguzi vinavyoongezeka nchini Libya dhidi ya wahamiaji wa Afrika kusini mwa jangwa la Sahara.

Mashirika hayo yanasema wahamiaji hao wa Kiafrika wanaowasili kwenye mpaka wa Libya kukimbia machafuko ni wachache na hii huenda ikawa ishara kwamba wengi wao wanaogopa kuondoka katika nyumba zao na kukimbia kuelekea mipakani.

Adrian Edward kutoka shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR anasema msichana mdogo pia alibakwa miongoni vya visa wanavyotendewa wahamajia wa Kiafrika.

(SAUTI YA ADRIAN EDWARD)

UNHCR imeongeza kuwa hakuna ndege nyingi za kuwahamisha wahamiaji na hasa wanaotoka Asia hususani Bangladesh na wale wa Afrika Kusini mwa jangwa la sahara.