Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Karne ya 21 wanawake wanahitaji fursa sawa:Bachelet

Karne ya 21 wanawake wanahitaji fursa sawa:Bachelet

Katika karne ya 21 ili mwanamke aendelee anahitaji kupata fursa sawa katika njanya mbalimbali imesema UN women.

Kimataifa maadhimisho ya 100 ya siku ya wanawake duniani yanafanyika mjini Monrovia nchini Liberia ambako Rais Ellen Johnson Sirleaf mwanamke wa kwanza kuwa Rais Afrika kwa ushirikiano na mkuu wa UN Women rais wa zamani wa Chile Michelle Bachelet wanazungumzia umuhimu wa uongozi wa wanawake katika kuendeleza demokrasia, kukuza uchumi na ujenzi mpya wa jamii baada ya machafuko na elimu.

(SAUTI YA MICHELLE BACHELET)

Bi Bachelet pia atazindua mpango maalumu wa kuandaa masoko kwa ajili ya wanawake , mpango unaofadhiliwa na UN Women.

Naye mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Navi Pillay akitoa ujumbe maalumu wa siku hii amesema machafuko yanayoendelea hivi sasa Mashariki ya Kati na Afrika yanaonyesha pengo lililopo katika uwepo wa elimu na fursa ya ajira na haki.

(SAUTI YA NAVI PILLAY)