Ushiriki wa wanawake katika kilimo utasaidia:FAO

7 Machi 2011

Shirika la chakula na kilimo duniani FAO leo imezindua ripoti ya mwaka 2011 ya hali ya chakula na kilimo.

Akizindua ripoti hiyo mkurugenzi mkuu wa FAO Dr Jacques Diouf amesema  ripoti hiyo inajikita katika jukumu la wanawake kwenye kilimo, na kuonyesha ni jinsi gani kukabiliana na matatizo ya kutokuwepo na usawa katika sekta ya kilimo kunavyoweza kusaidia kuinua uzalishaji wa chakula na kupunguza tatizo la njaa.

Wakati huohuo FAO imesema bei ya chakula imepanda kwa mwezi wa nane mfululizo na kuchangia kupanda kwa gharama za bidhaa zingine pia. Shirika hilo linasema kupanda kwa bei ya mafuta kusikotarajiwa kunaongeza hali mbaya iliyopo ya gharama za juu za chakula kwenye soko la dunia. George Njogopa na ripoti kamili.

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter