Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mratibu wa UM alezea hofu ya athari za machafuko Abyei

Mratibu wa UM alezea hofu ya athari za machafuko Abyei

Mratibu wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan George Charpentier ameelezea hofu yake juu ya athari za mapigano ya karibuni ya jimbo la Abyei kwa raia wa eneo hilo.

Amesema tangu kuzuka kwa mapigano hayo Februari 27 wakazi wengi wa Abyei wamekimbilia vijiji vya jirani wengine hadi eneo la Agok kilometa 40 Kusini mwa Abyei ambako wanapata msaada wa malazi kutoka kwa ndugu na jamii.

Wafanyakazi wa misaada wa UM na NGO's wanatathimini hali halisi na mahitaji ya maelfu ya watu wanaokimbia na wako tayari kutoa msaada kwenye eneo la Agok na Abyei kwenyewe hasa chakula, malazi, maji, vifaa vya usafi na madawa. Mratibu huyo amezitaka pande zote kuheshimu makubaliano ya Kadugli ya Januari 13 na 17 na makubaliano ya Abyei ya March 4 ya kutowaweka raia kwenye hatari.