Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM yaendelea kusafirisha wahamiaji wanaokimbia Libya

IOM yaendelea kusafirisha wahamiaji wanaokimbia Libya

Maelfu ya wahamiaji waliokimbia Libya wako kwenye mpaka baina ya Libya na Tunisia wakisubiri kusafirishwa na shirika la kimataifa la wahamiaji IOM.

Kwa mujibu wa shirika hilo hadi sasa maelfu ya wahamiaji waliokuwa wakifanya kazi nchini humo kutoka Misri wamerejeshwa makwao, na wengine kutoka Bangladesh, India, Pakistan na Afrika wanaendelea kusafirishwa. Hata hivyo kuna baadhi ya wahamiaji ambao baada ya kukimbia Libya hawajui wapi watakapopelekwa kutokana na kwamba nchi zao zinakabiliwa na machafuko.

Wahamiaji hao ni pamoja na wa kutoka Eritrea na Somalia. Mmoja wao ni Mohamed Abdallah miongoni mwa Wasomali 300 walioko kwenye mpaka wa Al Jadir ras Jadil.

(SAUTI YA MOHAMED ABDALLAH)