ombi la dola milioni 160 limezinduliwa na UM na washirika wake kuisaidia Walibya

7 Machi 2011

Katika kukabiliana na matatizo yanayoikumba Libya hivi sasa ambayo yamesababisha watu zaidi ya 190,000 kukimbilia nchi jirani za Tunisia, Misri na Niger, Umoja wa Mataifa , shirika la kimataifa la wahamiaji IOM na mashirika mengine ya misaada wamezindua ombi la kikanda la msaada kwa ajili ya matatizo ya Libya.

Dola milioni 160 zinahitajika ili kukidhi mahitaji ya maelfiu ya watu wanaokimbi machafuko na walioathirika nchini Libya katika kipindi cha miezi mitatu ijayo.

Akizungumzia ombi hilo la msaada huo mratibu wa masuala ya dharura ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa Valarie Amos aliyezuru mpaka baiana ya Libya na Tunisia mwishoni mwa wiki amesema ombi hili ni kutokana na mipango ya hali tunayoiona kwamba watu 400,000 wanakimbia Libya, wakiwemo 200,000 ambao wameshaondoka na wengine 600,000 walioko ndani ya Libya wanatarajiwa kuhitaji msaada wa aina mbalimbali.

(SAUTI YA VALARIE AMOS)

Ombi hilo la fedha litasaidia katika gharama za kuratibu makambi na kuyaongoza, katika usalama wa chakula, lishe, huduma za afya, maji, usafi, ulinzi, malazi na masuala ya kiufundi.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa UNGA76 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter