Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Libya yateua balozi mpya kuiwakilisha kwenye UM

Libya yateua balozi mpya kuiwakilisha kwenye UM

Serikali ya Libya leo imesema imeteua balozi mpya kuiwakilisha nchi hiyo kwenye Umoja wa mataifa.

Aliyeteuliwa ni Ali Abdussalam Treki ambaye kwa sasa ni waziri wa mambo ya nje na Rais wa zamani wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa.

Libya tayari inaye balozi kwenye Umoja wa Mataifa ambaye hivi karibuni hivi karibuni amejiepusha na utawala wa Rais Muammar Qadhafi baada ya kutoa kauli za kuukosoa vikali utawala wa Libya.