Raia zaidi ya 60 wauawa mjini Moghadishu Somalia

4 Machi 2011

Raia 62 wameuawa na wengine zaidi ya 230 kujeruhiwa katika kipindi cha wiki mbili kufuatia mapigano makali mjini Moghadishu Somalia.

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu masuala ya kibindamu OCHA limesema mapigano hayo yamezuia kupelekwa kwa misaada ya kibinadamu kwenye mji mkuu wa Somalia Moghadishu.

Somalia imekuwa bila serikali kuu inayofanya kazi kwa zaidi ya miongo miwili sasa na majeshi ya serikali ya mpito yanaendelea kupambana na wanamgambo wa Al-Shabaab.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa UNGA76 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter