Ban ataka vijana kutyumia mtandao kusaidia jamii

4 Machi 2011

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amewataka vijana ulimwenguni kote kutumia vyema fursa zinazopatikana kwenye teknolojia ya habari pamoja na internet kubuni mambo yatakayoleta manufaa kwa jamii na siyo vinginevyo kwani amesisitiza kuwa mitandao ya tovuti ni nyenzo yenye ushawishi mkubwa wa kuleta maendeleo.

Katika ujumbe wake alioutoa kwenye mkutano wa 35 wa shule za kimataifa unaoratibiwa na Umoja wa Mataifa, Ban amesema kuwa mitandao kama wavuti inaweza kutumika vyema ili kusadia kufikia shabaya ya malengo ya maendeleo ya mellenia.

Amesisitiza kuwa mitandao ya wavuti inaendelea kusalia kama chombo chenye nguvu na ambacho kinaweza kutumiwa vyema ili kuleta msaada kwa jamii. Vijana kutoka shule 48 wakiziwakilisha nchi 19, wanakutana kwenye mkutano huo wa siku mbili kwa ajili ya kubadilishana ujuzi na uzoefu kwenye maeneo

mbalimbali.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa UNGA76 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter