Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Shirika la Grandmothers la Argentina lapata tuzo ya amani ya UNESCO

Shirika la Grandmothers la Argentina lapata tuzo ya amani ya UNESCO

Shirika lisilo la kiserikali la Argentina liitwalo Grandmathers of the Plaza de Mayo, limetunukiwa tuzo ya amani ya shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni UNESCO.

Shirika la Grandmothers kwa zaidi ya miaka 30 limekuwa likifanya kazi ya kuzitafuta familia za watoto waliotekwa au kupotea wakati wa utawala wa kijeshi wa kidikteta nchini Argentina.

Majaji wa tuzo hiyo ya amani iitwayo "Felix Houphouet-Boigny" wanaokutana mjini Paris wamelitunukia tuzo hiyo shirika la Grandmothers of the Plaza de Mayo kwa vita vyao vya bila kuchoka kupigania haki za binadamu na amani na kwa kupinga ukandamizaji, ukosefu wa haki na wanaokwepa sheria.

Tuzo hiyo ambayo imepewa jina la Rais wa kwanza wa Ivory Coast ilianzishwa na UNESCO mwaka 1989. Washindi wa tuzo hilo shirika la Grandmothers lilianzishwa mwaka 1977 na nia yake ni kuhakikisha ukiukaji wa haki za watoto hautokei tena nchini Argentina.