Skip to main content

Mtalaamu wa haki za binadamu kutathimini hali Sudan Kusini

Mtalaamu wa haki za binadamu kutathimini hali Sudan Kusini

Mtaalamu huru kuhusu hali ya haki za binadamu nchini Sudan Mohamed Chande Othman atazuru Sudan Kusini na jimbo la Abyei ili kupata taarifa kuhusu kura ya maoni ya Sudan Kusini na masuala muhimu yanayohusiana na mkataba wa amani wa 2005.

Katika ziara yake hiyo ya pili nchini Sudan itakayoanza Jumapili Machi 6 hadi Machi 13 Bwana Othman atajadili na viongozi wa serikali mjini Khartoum kuhusu hali ya watetezi wa haki za binadamu .

Atafika pia Darfur kutathimini hali ya haki za binadamu baada ya mapigano ya hivi karibuni. George Njogopa na taarifa kamili.

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)