Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

FAO na OIE kusaidia kukabili ugonjwa wa miguu na midomo

FAO na OIE kusaidia kukabili ugonjwa wa miguu na midomo

Jopo la wataalamu wa mifugo kutoka shirika la chakula na kilimo FAO na shirika la kimataifa la afya ya wanyama OIE wamewasili Korea Kaskazini kusaidia wataalamu wa afya nchini humo kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa wa miguu na midomo kwa nguruwe na ng\'ombe.

Lengo la ziara yao ni kutathimini hali halisi ili kutoa taratibu za kufwatwa na msaada wa kiufundi kwa maafisa wa afya ya mifugo wa Korea ya Kaskazini, msaada utakaowawezesha kuudhibiti mlipuko huo na kuzuia usisambae zaidi.

Timu ya FAO na OIE pia itaisaidia nchi hiyo kwa mipango ya muda mrefu ya kuzuai ugonjwa huo. Jopo hilo litakuwepo nchi Korea ya Kaskazini kwa muda wa wiki mbili.