Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM waiomba radhi Belarus kwa kuituhumu kukiuka vikwazo vya silaha

UM waiomba radhi Belarus kwa kuituhumu kukiuka vikwazo vya silaha

Umoja wa mataifa umeomba radhi serikali ya Belarus ambayo hapo awali ilituhumiwa

kuwa ilikiuka vikwazo vya kimataifa vilivyowekwa kwa utawala Laurent Gbagbo wa

Ivory Coast, aliyepigwa marafuku kusambaziwa silha za aina yoyote.

Mkuu wa vikosi vya kulinda amani vya umoja wa mataifa nchini humo Alain Le Roy, amesema kuwa tuhuma zilitolewa dhidi ya Belarus hazikuakisi ukweli wa tukio na kwa maana hiyo umoja wa mataifa unaiomba radhi juu ya madai hayo.

Belarus ilituhumiwa kwamba imekwenda kinyume na tamko la kuwekwa vikwazo kwa Gbagbo baada ya kusambaza silaa kadhaa ikiwemo helikopta.

Katika mkutano wake na waandhishi wa habari, mkuu huyo wa vikosi vya Umoja wa mataifa amesema kuwa maafisa wa Umoja wa Mataifa walipotoshwa kwa kupewa taarifa za uwongo ambazo zilidai kuwa Belarus imeanza kusambaza silaa zake huko Ivory Coast.

Hata hivyo pande zote zimeafikiana kuendelea kuhakikisha vikwazo vilivyowekwa

dhidi ya Gbagbo havikiukwi.