UM wazindua ofisi kuzisaidia nchi za Afrika ya Kati

3 Machi 2011

Umoja wa mataifa leo umefungua ofisi maalumu kwa ajili ya kutoa msukumo wa kisiasa kwa kuimarisha hali ya amani na kuzua uwezekano wa kutokea machafuko katika nchi za afrika ya kati.

Ofisi hiyo pia itakuwa na jukumu la kukabiliana na changamoto kwenye maeneo ya mipakani ambako kuna wimbi kubwa la usafirishaji wa magendo wa silaa pamoja na magenge ya uhalifu.

Akizungumza kwenye sherehe za uzinduzi wa ofisi hiyo mjini Libreville, Gabon, mwakilishi wa Katibu Mkuu anayehusika na masuala ya siasa B. Lynn Pascoe amesema kuwa kilio cha muda mrefu kutoka kwa serikali za eneo hilo sasa kimepatiwa

ufumbuzi.

Ofisi hiyo inayojulikana kama UNOCA itafanya kazi kwa muda wa miaka miwili na mwakilishi wake anatazamiwa kuteuliwa na Katibu Mkuu Ban Ki-moon.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter