Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mapigano Abyei yauwa zaidi ya 100:UNMIS

Mapigano Abyei yauwa zaidi ya 100:UNMIS

Maafisa wa serikali ya Sudan wamesema maefu ya wanawake na watoto wamekimbia kwenye jimbo la Abyei nchini Sudan lililoko kwenye mpaka baina ya Kaskazini na Kusini kufuatia mapigano yaliyouwa watu zaidi ya 100.

Abey kwa muda imeonekana kama ni amana kwa pande zote mbili za Kusini na Kaskazini mwa Sudan, jimbo hilo liliahidiwa kupiga kura ya maoni kuamua endapo litajiunga na Kaskazini au Kusini iliyoamua kujitenga mwezi Januari mwaka huu na itakuwa taifa jipya la Afrika mwezi Julai.

Kwa mujibu wa msemaji wa mpango wa Umoja wa Mataifa Sudan UNMIS Bi Hua Jiang wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa Abyei wamethibitisha kushuhudia mazishi ya watu 33 waliokufa kwenye mapigano ya jana Jumatano.

Amesema wanawake na watoto 300 wamekimbilia kwenye mji wa Agok kutoka Abyei huku wengine 60,000 wakazi wa Abyei walikimbia mwaka 2008 baada ya majeshi ya Sudan na washirika wao kuvalia jimbo hilo.