Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hofu ya kupanda kwa bei ya chakula yaongezeka:FAO

Hofu ya kupanda kwa bei ya chakula yaongezeka:FAO

Shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa FAO leo limesema bei ya chakula imepanda kwa mwezi wa nane mfululizo na kuchangia kupanda kwa gharama za bidhaa zingine pia.

Shirika hilo linasema na kupanda kwa bei ya mafuta kusikotarajiwa kunaongeza hali mbaya iliyopo ya gharama za juu za chakula kwenye soko la dunia. George Njogopa na ripoti kamili.

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)

Ikiangazia zaidi hali hiyo FAO imetoa takwimu zinazoonyesha kuwa ongezeko la safari hii ni la kiwango cha juu zaidi tangu kuanza mfumo wa ufuatiliaji wa mwenendo wa bei mwaka 1990.

Bidhaa muhimu kama ngano, mpunga pamoja na mahindi zijaachwa nyuma kwenye ongezeko hilo, zikishuhudiwa zikipanda kwa asilimia 3.7, kiwango ambacho ni cha juu kuwahi kufikiwa katika miaka ya hivi karibuni.

Hata hivyo FAO inakadiria kwamba hali inaweza kubadilika katika msimu wa baridi

ambako uzalishaji wa ngano unategemewa kupanda kwa asilimia 3.Hali hii inazamiwa

zaidi kujitokeza katika nchi ambazo ni wazalishaji wakubwa wa ngano.