Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Somalia yatakiwa kutekeleza makubaliano ya Djibouti

Somalia yatakiwa kutekeleza makubaliano ya Djibouti

Serikali ya mpito ya Somalia na bunge la nchi hiyo lililojiongezea muda wa miaka mitatu wametakiwa kutekeleza makubalino ya amani ya Djibouti.

Hayo yamesisitizwa kwenye mkutano maalumu uliomalizika leo mjini Acca Ghana na kujumuisha bunge la Afrika, Umoja wa Mataifa na bunge la serikali ya mpito ya Somalia. Ajenda kubwa ni kulisaidia bunge la Somalia kuweza kutimiza wajibu wake katika kipindi hiki cha mpito.

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia Balozi Augustine Mahiga aliyehudhuria mkutano huo anasema kuna mambo matatu bunge la Somalia linatakiwa kutekeleza.

(SAUTI YA AUGUSTINE MAHIGA)