Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mapigano Ivory Coast yanawaweka raia katika hatari:Pillay

Mapigano Ivory Coast yanawaweka raia katika hatari:Pillay

Kamishina mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Navi Pillay leo ameonya kwamba raia wako katika hatari kubwa kutokana na machafuko yanayoendelea mjini Abidjan Ivory Coast.

Bi Pillay akizungumza kwenye baraza la haki za binadamu mjini Geneva amesema janga la kibinadamu linaikumba nchi hiyo ambapo maelfu ya watu wanakimbia mapigano.

Pillay amesema anatiwa hofu na kuongezeka kwa ghasia na ukiukaji wa haki za binadamu nchini Ivory Coast. Umoja wa Mataifa unasema watu zaidi ya 200,000 wamekimbia mapigano makali yanayoendelea kwenye wilaya ya Abobo mjini Abidjan.