Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Waliobakwa DR Congo walipwe fidia:UM

Waliobakwa DR Congo walipwe fidia:UM

Jopo la Umoja wa Mataifa lililofuatilia visa vya ubakaji Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo leo limesema wanawake wa nchi hiyo ambao wamebakwa wanapaswa kulipwa fidia wakati wakiendelea kuteseka kutokana na kunyanyapaliwa na kutelekezwa.

Inakadiriwa kwamba wanawake 200,000 wamebakwa katika taifa hilo la Afrika ya Kati katika kipindi cha miaka 12 iliyopita ambayo imeghubikwa na vita.

Jopo hilo linalohusisha naibu kamishina mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa, waziri wa ulinzi wa zamani wa Finland, mwandishi wa ripoti ya UNIFEM kuhusu wanawake, vita na amani na mkurugenzi wa hospitali ya Pazi Bukavu Kivu Kusini, linasema mahitaji ya wahanga wa kubakwa waliowahoji hayajatimizwa hususani kwenye maeneo ya vijijini.

Maisha yao yameharibiwa na wanateseka sana kwa mujibu wa ripoti hiyo. Navi Pillay ni kamishina mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa akizungumzia ripoti hiyo amesema.

(SAUTI YA NAVI PILLAY)