IOM yahamisha wahamiaji Benghazi Libya
Juhudi za haraka za kusaidia kuwahamisha wahamiaji waliokwama Benghazi nchini Libya zinaendelea.
Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM limesema leo limeanza awamu ya kwanza ya kuwahamisha wahamiaji kutoka katika mji huo wa bandari.
Kipaumbele kimetolewa kwa wahamiaji 200 walio katika hatari hususani wanawake, watoto na wanaohitaji huduma za afya. Hadi sasa wahamiaji 5500 wamebainika kukwama katika maeneo mbalimbali ikiwemo bandarini na kwenye maghala na wengi ni raia wa Bangladesh, India, Sudan, Syria, Ghana na wachache kutoka nchi zingine.