Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mwakilishi wa UM Sudan alaani mapigano ya Abyei

Mwakilishi wa UM Sudan alaani mapigano ya Abyei

Mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan amelaani vikali mapigano ya hivi karibuni kwenye jimbo la Abyei.

Haile Menkerios ambaye pia ni mkuu wa UNMIS amesema mapigano hayo ni ukiukaji dhahiri wa barua na ari ya makubaliano ya Kadugli yaliyoafikiwa tarehe 13 na 17 Januar1 2011.

Menkerios amezitaka pande husika katika mapigano hayo kuchukua hatua ya kutekeleza makubalino ikiwa ni pamoja na kuanzisha kamati ya ngazi za juu ya utekelezaji wa makubaliano hayo na kuanza kutekeleza wajibu wake. Amesema kamati hiyo itatumika kama njia ya kudhibiti matukio kama hayo na kuhakikisha hayatokei tena.

Ameongeza kuwa UNMIS iko tayari kusaidia pande zote kufanikisha makubaliano hayo. Pia amezitaka pande zote mbili kupata suluhu ya jimbo la Abyei kama ilivyoahidiwa na Rais mwezi uliopita.