Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mauaji ya waziri Pakistan yalaaniwa:Pillay

Mauaji ya waziri Pakistan yalaaniwa:Pillay

Kamishina mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa mataifa Navi Pillay leo amelaani mauaji ya waziri anayehusika na masuala ya walio wachache nchini Pakistan bwana Shahbaz Bhatti ambaye ni kiongozi wa pili kuuawa tangu kuanza kwa mwaka huu kwa sababu ya kupinga sheria za nchi hiyo za kukashifu dini.

Bwana Bhatti aliuawa baada ya mtu mwenye silaha kushambulia gari lake mjini Islamabadi hii leo. Tarehe 4 Januari gavana wa Punjab Salman Taseer pia aliuawa mjini Islamabad baada ya mmoja wa walinzi wake kumpiga risasi kwa sababu ya kupinga sheria hizo.

Bi Pillay amesema mauaji hayo ni pigo kubwa kwa Pakistan na kwa hatma ya haki za binadamu, na kusema anatuai serikali itawashughulikia waliofanya mauaji hayo na kuzifanyia marekebisho sheria zake.