Skip to main content

Mpango mipya ya UN inalenga uhalifu wa kupangwa maeneo ya vita:UNODC

Mpango mipya ya UN inalenga uhalifu wa kupangwa maeneo ya vita:UNODC

Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayohusika na udhibiti wa madawa na uhalifu UNODC na idara ya Umoja wa Mataifa inayohusika na masuala ya kulinda amani DPKO leo wamezindua mipango maalumu ya kukabiliana na usafirishaji haramu wa mihadarati na mifumo mingine.

Kwa mujibu wa mkurugenzi mtendaji wa UNODC Yuri Fedotov mipango hiyo itahusiha nchi mbalimbali lakini amesema mradi wa majaribio utaanzia Afrika ya Magharibi ambako kunaonekana kuwa kitovu cha kusafirisha mihadarati.

(SAUTI YA YURI FEDOTOV)

Ameongeza kuwa pia ana mipango ya kwenda Afrika Mashariki akianzia Kenya na nchi jirani ambazo zitaweza kuisaidia UNODC kutathimini hali halisi na jinsi ya kuisaidia Kenya hasa katika suala la maharamia kwenye pwani ya Somalia. Na atazuru Somalia ambako UNODC inasaidia kuendesha kesi na kuwafunga maharamia waliokamatwa na majeshi ya kimataifa.