Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mapigano makali yaghubika Moghadishu:Mahiga

Mapigano makali yaghubika Moghadishu:Mahiga

Taarifa kutoka Moghadishu nchini Somalia zinasema mapigano makali yamekua yakiendelea kwa siku sita mfululizo kati ya vikosi vya serikali ya mpito na wanamgambo wa Ali-Shabaab.

Watu zaidi ya 40 wakiwemo wanajeshi wa kulinda amani wa muungano wa Afrika AMISOM, raia na wanamgambo wa Al-Shaabab wameuawa.

Katika mapigano hayo hata hivyo vikosi vya serikali ya mpito vimefanikiwa kuyadhibiti tena maeneo kadhaa yaliyokuwa yanashikiliwa na wanamgambo kama anavyofahamisha Balozi Augustine Mahiga mwakilishi wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia.

(SAUTI YA BALOZI MAHIGA)