Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mabadiliko Mashariki ya Kati na Afrika ya Kaskazini yatatoka ndani ya eneo hilo asema Ban na kuwa UM uko tayari kusaidia

Mabadiliko Mashariki ya Kati na Afrika ya Kaskazini yatatoka ndani ya eneo hilo asema Ban na kuwa UM uko tayari kusaidia

Baraza kuu la Umoja wa Mataifa limekutana leo mjini New York kutathimini na kupitisha mswada wa azimio la baraza la haki za binadamu la kuisitisha uanachama Libya.

Baraza la haki za binadamu lililokutana Geneva lilipitisha azimio tarehe 25 Februari la kusitisha uanachama wa Libya kwenye baraza hilo kutokana na machafuko yanayoendelea nchini humo yanayoelezewa kwenda sambamba na ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu.

Akizungumza kwenye kikao hicho maalumu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema anapongeza uamuazi wa baraza la haki za binadamu kwa kusitisha uanachama wa Libya na anaunga mkono uamuazi wa kutuma jopo la uchunguzi.

(SAUTI YA BAN KI-MOON)

Ban ameongeza kuwa mabadiliko Afrika ya Kaskazini na Mashariki ya Kati, lazima yatoke ndani ya eneo hilo. Naye mwakilishi wa Afrika katika kikao hicho ambayo ni nchi ya Mauritius imesema Afrika inasikitishwa na hali inayoendelea Libyia na kusema kundi la Afrika kwenye baraza la haki za binadamu linaunga mkono azimio lililopitishwa tarehe 25 Februari kwa sababu haki za uhuru wa kujieleza, mkusanyiko wa amani na uhuru wa kuandamana vinatakiwa kutekelezwa chini ya sheria za Umoja wa Mataifa na chini ya azimio la haki za binadamu la Afrika lililopitishwa mwaka 1981.

Imeongeza kuwa na wakati jumuiya ya kimataifa inaungana kulaani ukiukaji wa haki za binadamu Libya basi iungane pia katika kuisaidia nchi hiyo kukabiliana na changamoto zilizo mbele yao.