UM waongeza nguvu kuwasaidia waathirika Libya:OCHA

1 Machi 2011

Wakati hali ikizidi kuchacha nchini Libya huku makundi ya watu wanaunga mkono utawala wa Muammar Al-Qadhafi ukiwaandamana wakimbizi na kuongeza hali ya wasiwasi juu ya usalama, Umoja wa Mataifa umezidisha nguvu zake ili kuwasaidia makundi makubwa ya wakimbizi wanaomiminika kwenye maeneo ya mipakani pamoja na maeneo ya ndani ya nchi.

Mkuu wa shirika la umoja wa mataifa linalohusika na misaada ya kiutu OCHA, Valerie Amos amesema leo kuwa ofisi yake imelazimika kutuma timu ya wataalamu kwenda Cairo ambao watatoa uangalizi na msaada wa karibu kwa kikosi kingine cha umoja huo kilichopo Tripol.

Hali jumla nchini Libya siyo ya kutia matumaini mnamo wakati kunashuhudiwa kuzorota kwa hali ya usalama na kukosekana kwa huduma nyingine muhimu kama madawa na chakula. OCHA imesema kuwa inafuatilia kwa karibu hali jumla ya mambo nchini Libya, na inafanya juu chini kuhakikisha kwamba inawafikia waathirika wa machafuko hayo.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter