Tusiwasahau na wengine wanaokumbwa na machafuko:IOM

1 Machi 2011

Shirika la Umoja wa mataifa la uhamiaji IOM limeonyesha wasiwasi kutokana na kuendelea kuongezeka kwa wakimbizi wa ndani nchini Ivory Coast ambayo imetumbukia kwenye mkwamo wa kisiasa tangu duru ya pili ya uchaguzi wa rais mwaka jana.

IOM imesema kuwa wakati wakimbizi hao wakiendelea kuongezeka hadi kufikia zaidi ya 129,500, matumaini ya kuimarika kwa hali ya usalama yanaendelea kupungua jambo linalozidisha wasiwasi mwingine.

Shirika hilo limezitaka jumuiya za kimataifa kutolisau bara la afrika kwani inakabiliwa na changamoto ya kuendelea kuongezeka kwa wakimbizi hao wa ndani.

Ripoti zaidi zinasema kuwa wakimbizi wengi wa Ivory Coast wanakatiza mpaka na kuingia nchi jirani ya Liberia, huku wengine mamia kwa maelfu wakiwa mtawanyikoni kwenye miji mbalimbali ikiwemo mji mkuu wa Abidjan

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter