Zimbabwe imetakiwa kuwaachilia wanaharakati waliokamatwa

Zimbabwe imetakiwa kuwaachilia wanaharakati waliokamatwa

Serikali ya Zimbabwe imetakiwa kuwaachilia kundi la wanaharakati wa kijamii walioshitakiwa kwa uhaini baada ya kujadili matukio yanayoendelea Misri na Libya.

Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Navi Pillay amesema kuwakamata wanaharakati hao 45 ni dalili kwamba demokrasia nchini Zimbabwe bado iko mbali.

Bi Pillay ameitaka serikali kutimiza ahadi yake ya kumaliza ukandamizaji na kutovumiliana. George Njogopa anaripoti.

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)