Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

LRA waendelea kushambulia Mashariki mwa DRC:UNHCR

LRA waendelea kushambulia Mashariki mwa DRC:UNHCR

Ghasia na mashambulizi dhidi ya raia yanayofanywa na kundi la Lords Resistance Army (LRA) la Uganda Kaskazini Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ymaeendelea kuongeza hofu kwa mujibu wa shirika la kuhudumia wakimbizi UNHCR.

Shirika hilo linasema tangu Januari mwaka huu LRA imezidisha mashambulizi kwenye jimbo la Oriental na kuuwa watu 35, kuteka 104 na kuwafanya zaidi ya 17,000 kuzikimbia nyumba zao.

Kwa kipindi cha miezi miwili UNHCR inasema kumefanyika matukio ya mashambulizi 52 hali ambayo imekuwa kikwazo kikubwa kwa kazi za mashirika ya kibinadamu na kutoa msaada. Melisa Fleming ni msemaji wa UNHCR.

(SAUTI YA MELISA FLEMING)