Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wafuasi wa Ouattara wamekwama Abijan:UNHCR/UNICEF

Wafuasi wa Ouattara wamekwama Abijan:UNHCR/UNICEF

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limesema linaendelea kutiwa hofu na hali ya raia ambao ni wafuasi wa Alassane Ouattara nchini Ivory Coast ambao wamekwamba kwenye wilaya ya Abobo mjini Abijan kufuatia mapigano ya hivi karibuni.

Kwa mujibu wa UNHCR mji huo ulio na watu milioni 1.5 bado umeghubikwa na hofu huku maelfu ya watu wamekimbia, lakini makundi yenye silaha yakiarifiwa kuwazuia baadhi ya watu kuondoka na UNHCR imesitisha ujenzi wa kambi ya wakimbizi.

Shirika la kuhudumia watoto UNICEF linasema wanawake na watoto ndio waathirika wakubwa na maradhi ya surua na homa ya manjano yameongeza adha. Shirika hilo linasema watoto wengi wamepata chanjo kama anavyofafanua msemaji wa UNICEF Marixe Mercado

(SAUTI YA MARIXE MERCADO)