Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkuu wa haki za binadamu aionya serikali ya Yemen

Mkuu wa haki za binadamu aionya serikali ya Yemen

Kamishina mkuu wa wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Navi Pillay ameionya serikali ya Yemen kwa ghasia na ukandamizaji dhidi ya wanaofanya maandamano ya amani nchini humo na ameitaka serikali kulinda haki za waandamanaji na waandishi wa habari chini ya sheria za kimataifa.

Akinukuu ripoti kwamba waandamanaji wa upinzani wameiita siku ya leo kama siku ya hasira, kamishina mkuu amezitaka pande zote kujizuia na kuheshimu haki za uhai wa watu na uhuru wa kujieleza na kukusanyika kwa amani.

Amesema watu wana haki ya kuelezea machungu yao na madai yao kwa serikali na ametaka ghasia dhidi ya waandamanaji sikomeshwe mara moja baada ya waandamanaji kadhaa kuuawa na kujeruhiwa.