Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban Ki-moon na Obama wajadili hali ya Libya

Ban Ki-moon na Obama wajadili hali ya Libya

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon na Rais wa Marekani Barak Obama wamekutana mjini Washington D.C na kujadili hali ya Libya.

Ziara ya Ban imekuja baada ya baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kupitisha azimio mwishoni mwa wiki la kumuwekea vikwazo Rais wa Libya Muammar Qadhafi. Kwa mujibu wa msemaji wa Umoja wa Mataifa Martin Nesirky ni kwamba Katibu Mkuu na Rais Obama watajadili njia mbalimbali za kusaidia hali inayozidi kuzorota ya machafuko nchini Libya.

(SAUTI YA MARTIN NESIRKY)

"Ni dhahiri kuna maendeleo makubwa yaliyojitokeza kwa mwishoni mwa wiki baraza la usalama kupitisha azimio hili bila kupingwa na itakuwa ni muhimu kwa Katibu Mkuu na Rais wa Marekani kuweza kulizungumzia na utekelezaji wake. Bila ya shaka kwa sasa kuna jambo kubwa la kutilia mkazo, hali ya kibinadamu pamoja na mipango ya usalama. "

Katibu Mkuu pia anazuru makumbusho ya mauaji ya Holocaust D.C katika mipango ya Umoja wa Mataifa ya kukumbusha nia yake ya kuheshimu na kulinda haki za binadamu.