Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban akaribisha mafanikio yaliyofikiwa Gabon

Ban akaribisha mafanikio yaliyofikiwa Gabon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amepongeza hatua iliyofikiwa nchini Gabon ambayo imewawezesha kundi la watu kadhaa waliokuwa wakipata hifadhi kwenye majengo ya umoja huo kujerea makwao kwa hiari na amani.

Watu hao akiwemo kiongozi mkuu wa chama cha upinzani Andre Mba Obame walikimbilia kwenye majengo ya shirika la maendeleo la umoja wa mataifa UNDP mjini Libreville kwa ajili ya kuomba hifadhi tangu January 25.

Ban amempongeza rais Ali Bongo Onbimba wa Gabon kutokana na ushirikiano wake na umoja wa mataifa kutanzua hali iliyojitokeza hivi karibu ambayo ilisababisha wananchi hao kukimbia. Amesema anamatumaini makubwa kwa serikali iliyopo madarakani itaendelea kuweka zingatio la kuimarisha hali ya amani na kuondosha tofauti za kisiasa zilizojitokeza hivi karibuni.