Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vikosi ya UNOCI vyashambuliwa Ivory Coast

Vikosi ya UNOCI vyashambuliwa Ivory Coast

Askari kadhaa wa umoja wa mataifa wa kulinda amani nchini Ivory Coast wameshambuliwa na kujeruhiwa.

Katika tukio hilo ambalo limejiri katika eneo lijulikanalo Abobo kaskazini mwa mji wa Abidjan askari watutu walijeruhiwa na kuharibiwa pia magari manne ya vikosi hivyo.

Taarifa iliyotolewa na vikosi hivyo, imelaani vikali matukio kama hayo ambayo yanadaiwa kufanywa mwishoni mwa wiki na vikosi vinavyounga mkono utawala wa Laurent Gbagbo ambaye hatambuliki kwenye jukwaa la kimataifa.

 Matokeo ya uchaguzi mkuu wa mwezi Novemba mwaka jana, ndiyo yaliyozusha mkwamo wa kisiasa nchini Ivory Coast, huku pande mbili zikiendelea kurumbana.