Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watu wa Libya kuamua hatima yao: waziri wa Italia

Watu wa Libya kuamua hatima yao: waziri wa Italia

Watu wa Libya wanahitaji msaada wa kimataifa wakati wakijaribu kupata njia mbadala ya serikali ya Muammar Qadhafi.

Hayo yamesemwa na waziri wa mambo ya nje wa Italia Franco Frattin alipozungumza na waandishi wa habari kufuatia mkutano wa baraza la haki za binadamu mjini Geneva. Ameongeza kuwa Muungano wa Ulaya unatambua kuwa serikali ya Libya imepoteza udhibiti wa baadhi ya sehemu za nchi hiyo kufuatia machafuko na maandamano ya wanaoipinga serikali.

Bwana Frattin amesema ni juu ya watu wa Libya kuamua hatma yao. Amesema ni juu ya watu wa Libya kuamua nini cha kufanya kuhusu nchi yao lakini ni juu ya jumuiya ya kimataifa kwanza kufanya kila linalowezekana kusitisha ghasia, kulaani utawala wa Qadhafi, kuutenga na kusaidia watu wan chi hiyo wanaohitaji msaada.

Bwana Frattin amesema Marekani, Ufaransa, Italia, Ujerumani na Uingereza wamejadili jinsi ya kuratibu vikwazo dhidi ya Libya vilivyowekwa na baraza la usalama siku ya Jumamosi.