Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakati umefika kwa Qadhafi kuondoka:Clinton

Wakati umefika kwa Qadhafi kuondoka:Clinton

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Hilary Clinton akizungumza kwenye mkutano wa baraza la haki za binadamu amesema macho yote hii leo yanajikita kwa Libya.

Clinton amesema serikali ya Libya inatumia silaha nzito dhidi ya raia, inatumia askari maluki, inawakamata watu na pia kuwatesa. Bi Clinton amesema ukiukwaji wa haki za binadamu nchini Libya haukubaliki na hautavuliwa.

(SAUTI YA HILARY CLINTON)

Pia ameelezea matumaini kwa muungano wa Afrika kwamba utafuata nyayo za wenguine kwa kuchukua hatua za kushughulikia hali ya Libya. Amesema leo pia Rais Barak Obama na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon wanakutana na wataendelea kuchukua hatua dhidi ya Rais Gaddafi na kutoa msaada wa kibinadamu unaohitajika kwa mamilioni ya watu.